Mukama akiongea na waandishi wa habari.
Alisema kuwa mfumo huo unawanyima fursa wapiga kura wa mshindi wa pili wa uchaguzi, kupata uwakishi katika mambo mazito ya mendeleo.
Mukama alisema hayo jijini Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungwa kwa mkutano wa uwezeshaji wa vyama vya siasa kifedha.
“Suala hili limekuwa likizungumza sana katika vyama kwamba ili ushinde lazima uwe na asilimia kubwa kwenye uchaguzi, naweza kusema ni kweli au sio kweli, lakini sheria ya vyama inazingatia wingi wa kura, hivyo mfumo wa uchaguzi sio mzuri ambao mshindi hushinda kwa kura,” alisema.
Kwa mujibu wa Mukama, mfumo huo ambao humpa mshindi mtu aliyesimamishwa na chama, badala ya chama husika na kuwanyima fursa wapiga kura wa mgombea mwingine kutoa maoni yao baada ya kushindwa katika uchaguzi.
Akitolea mfano wa kiti cha ubunge, alisema wabunge wengi huchaguliwa kwa mfumo huo badala ya kuteuliwa na chama husika ambapo mwisho wa uchaguzi mshindi huamriwa kwa kuangalia uwingi wa kura alizopata.
Mukama alibainisha kuwa hatua hiyo inasababisha na kuzindisha mgawanyiko miongoni mwa wananchi na hivyo akataka kuwa na utaratibu mpya wa kuchaguliwa chama pamoja na kumpata mshindi kwa uwiano wa kura.
Awali, Mwenyekiti wa chama cha CUF, Ibrahim Lipumba, alisema mkutano huo umekuwa wa manufaa kwao kutokana na kujifunza mambo mbalimbali kuhusu vyama vya siasa.
Chanzo Tanzania Daima