Showing posts with label Habari. Show all posts
Showing posts with label Habari. Show all posts

Monday, April 24, 2017

Tech News: Dell watangaza Aina mpya ya Monitor HDR



Kampuni inayojishughulisha na utngenezaji wa kompyuta na vifaa vya kompyuta ya Dell imetangaza kutoa kioo chenye uwezo wa kuonesha video za 4K yaani HDR. Hii ni aina ya kioo au Monitor inayotumika kwenye kompyuta yenye uwezo wa HDR 4K hii ni teknolojia ya kisasa hasa kwenye mambo ya video. Inatarajiwa kuwa madukani kuanzia mwezi wa tano mwaka huu wa 2017. Bei yake ni Dola za kimarekani 1,999.99

  
Credit to The Verge

Monday, June 6, 2016

Juisi ya Limau kwa Afya yako





 
Na Mwandishi Wetu.

Wataalamu wa afya na tiba asili wanasema pindi unapokuwa unatumia juisi ya limau kama mbadala wa chai husaidia kusafisha figo, kufanya mwili umeng'enye chakula vizuri, kuupatia mwili vitamini c na kuufanya mwili kupata hamu ya kula pia inakukinga na maradhi yanayosababishwa na sukari tunayoitumia kwenye chai.



Vilevile limao mbali nakutumiwa kama juisi hutumika na kupunguza ukali wa kilevi kwenye pombe kali kama vile whisky, spirits, gins au brandy pindi unapokuwa unaichanganya inakufanya usijikie vibaya au usilewe sana wala kudhuru mwili wako pindi unapoinywa hiyo pombe.

 

Friday, June 3, 2016

Visa waja na pete ya manunuzi

 Kampuni ya visa inayojihusisha na huduma ya kutoa kadi za manunuzi na malipo imetengeza pete maalum inayofanya. Kazi kama kadi za manunuzi ambapo itatolewa kwa majaribio huko brazil kwa wanamichezo washiriki wa michuano ya olimpiki mwaka huu.

Credit to Theverge.com

Thursday, June 2, 2016

App ya Instagram na Matangazo ya Biashara

http://img-s-msn-com.akamaized.net/tenant/amp/entityid/BBtI5HM.img?h=410&w=728&m=6&q=60&o=f&l=f&x=604&y=304

Kampuni ya Facebook kutoka marekani imeongeza wigo wa matangazo kupitia app yake ya kushare picha na video fupi ya Instagram kama njia nyingine ya kutangaza biashara mbalimbali za mtandaoni.

Kupata habari kwa undani zaidi ingia >>> HAPA >>>

Google kupitia OS yao ya Adroid Kuiboresha zaidi

http://img.s-msn.com/tenant/amp/entityid/BBjrScm.img?h=414&w=624&m=6&q=60&u=t&o=t&l=f&f=jpg&x=239&y=175

Kampuni ya Google ya nchini Marekani inampango wa kuiboresha Operating System yao ya simu ya Android kuifanya bora zaidi ili kuweza kushindana na Apple Inc wanaotengeneza simu za Iphone.

Kujua habari zaidi ingia  >>> HAPA

Friday, May 13, 2016

Ugeni wa mabasi ya haraka waendelea kutesa wasafiri


Monday, January 4, 2016

Msanii Chipukizi Mequiz as Brain anaetamba na Wimbo wa Happy Day..

Picha hii ni cover ya wimbo wa Happy Day. Picha kwa hisani ya ActionRec Blog.

Msanii anayekuja kwa kasi katika muziki huu wa kizazi kipya wa kufokafoka anayejulikana kwa jina la Mequiz as Brain aliachia wimbo huu siku chache zilizopita. Msanii huyu aliongea na Blog hii nakusema kuwa atafanya mambo mengi mwaka huu wa 2016 katika tasnia hii ya muziki pia alisema kuwa ataachia video ya wimbo huu siku zijazo.

Wimbo huu kawashirikisha wakali wa muziki wa kizazi kipya Mjini hapa Kahama toka kundi la Nyasubi Texas na kufanya kazi na studio za Action Records. Kuupakua wimbo huu bonyeza link hii >>>HaPa<<<

Sunday, December 20, 2015

Heshima kwa Kina mama wote..

 
Nilikuwa nawadharau sana wanawake niliwaona kama viumbe dhaifu wasio na akili na hii ilitokana na mazingira niliyokulia ambapo mwanamke anadharaulika na kubezwa.
Wiki iliyopita nilimpeleka mke wa kujifungua kwenye hospitali ya private ambapo hospitali hiyo ina utaratibu wa kumzalisha mwanamke mmewe wake akiwa pembeni anaangalia, aisee kuzaa ni shughuli asikwambie mtu nilitoka labour nduki mpaka sasa nikifikria kitendo kile nimeanza kuwaheshimu wanawake .
Kama hospitali zote zingelikuwa na utaratibu ule hakika wanaume tungewaheshimu wake zetu, mama zetu na wanawake wote kwa ujumla acha mama aitwe mama.

Credit to JamiiForums.com

Saturday, May 23, 2015

UWANJA MKUBWA ZAIDI DUNIANI


Rungrado Stadium , Pyongyang, Korea Kaskazini huu ndiyo uwanja mkubwa michezo duniani. Hutumika kwa michezo mbali mbali ikiwemo kandanda.

Ndiyo uwanja mkubwa zaidi duniani ambao hautumiwi kwa mbio za magari.
Una uwezo wa kuchukua watazamaji wapatao 150, 000. Ndiyo hutumiwa na timu ya Taifa ya Korea ya Kaskazini....


Duru zisizokuwa za soka zinadai kwamba ni katika uwanja huu ambapo majenerali kadhaa waliuawa kwa kuchomwa moto wakiwa hai baada ya kuhusishwa na jaribio la mapinduzi la kutaka kumuua kiongozi wa nchi hiyo, Kim Jong-il

Credit to: Baraka Mbolembole

Thursday, May 21, 2015

Uoga wa Raia wa Kitanzania Wakwamisha Mambo


Yako mambo mengi madogo madogo ambayo watu hutenda na kuleta mabadiliko. Lakini, kila wakati lazima pawepo msukumo ili kufanikiwa, iwe katika nyanja za elimu, afya bora, mazingira safi na mengineyo.
Hali ya mazingira wakati huu ina umuhimu zaidi kuliko ilivyokuwa siku za nyuma kutokana na mabadiliko ya tabia nchi pamoja na athari zake zisizofikirika katika maendeleo ya binadamu.
Wakati wanasayansi wanajadili uhusiano kati ya uunguzaji wa mafuta ya asilimwamba, kuongezeka kwa hewa ukaa na kupanda kwa halijoto duniani, Watanzania wanahitajika kuchukua hatua za haraka kurekebisha uharibifu mkubwa wa mazingira yao.
Ni zaidi ya miongo miwili tangu mfumo wa siasa za vyama vingi ulipoanzishwa Tanzania, lakini raia wa nchi hii bado si wepesi kuanzisha au kujiunga na vikundi vya hiari ambavyo vinaweza kuharakisha maendeleo na kuepusha mgogoro wa kimazingira ambao unaweza kutokea.
Shauku iliyoambatana na ushindi wa jumuiya za kiraia katika kuanzisha vyama vya siasa imefifia. Hata baadhi ya vyama vimepotea hivyo hivyo.
Lakini bado watu wanalalamika kuhusu ongezeko la umasikini; elimu duni; uhaba wa huduma bora za afya; unyanyasaji wa wanawake na watoto; ubaguzi wa kijinsia katika taratibu za kufanya maamuzi; ukosefu wa makazi bora; hali duni ya huduma za usafi wa mazingira na mambo mengine mengi katika mlolongo wa mapungufu katika maisha ya kila siku Tanzania.
Wakulima wadogo hawana imani tena na vyama vya ushirika. Katika mikoa ambapo vyama hivyo vilikuwa mhimili wa maendeleo kutokana na uuzaji wa mazao ya biashara hali imerudi nyuma baada ya kushuka kwa bei za mazao pamoja na uzalishaji.
Hali ni hiyo hiyo mijini ambako vyama vya ushirika wa walaji vilikuwa vimestawi kutokana na mafanikio ya kutetea haki za walaji na kuwasogezea bidhaa karibu. Wakati walaji wakiongezeka kila mwaka, vyama hivyo vimetoweka.
Mvua kubwa ziliponyesha wiki ya kwanza ya mwezi huu wa Mei katika ukanda wa pwani na kusababisha uharibifu uliotokana na mafuriko Dar es Salaam na Zanzibar, watu wengi walianza kutafakari wakijiuliza ni kitu gani kimevuruga mwenendo wa maisha. Zama zimepita ambapo jumuia zilijitoa kukabili changamoto kama hizo kabla ya kuomba msaada kutoka nje.
Kwa kiwango kikubwa mafuriko ya sasa ni changamoto kwa serikali kufanya matengenezo, kupanga na kujenga miundombinu inayofaa.
Maafisa wa serikali wamewaambia wakazi wa mabondeni ambayo hufurika wakati wa mvua wajijue wenyewe, kwa sababu mara kwa mara wamekaidi kufuata ushauri wa kuhamia sehemu za miinuko. Lakini waathirika pamoja na familia zao wanalia wapate msaada ambao haupatikani.
Wiki moja kabla ya mafuriko, wakazi wa mitaa ya Avocado, Kawe Beach and Mzimuni wilayani Kinondoni katika jiji la Dar es Salaam walitangazwa katika taarifa za televisheni kuwa ni mfano wa watu wanaojali kupendezesha mazingira yao.
Wana nia thabiti kutunza usafi wa mitaa, siyo tu kwa kuondoa taka lakini pia kuzuia madawa ya kulevya na uhalifu, vitu ambavyo vimeharibu sifa za maeneo mengi ya mijini na kuwanyima wananchi raha ya kujisikia kuwa na jumuiya zao wenyewe.
Wakati huo, mbunge wa jimbo la Ludewa kusini mwa Tanzania amefaulu kuwaunganisha wananchi, bila kujali vyama vyao vya siasa, wafanye kazi bila malipo kukamilisha mradi wa usambazaji umeme vijijini. Kwa kuwashawishi, ameweza kuwaongoza wafanye kazi ambayo italeta mabadiliko ya kudumu katika maisha baada ya vijiji vyao kupata umeme kutoka gridi ya taifa.
Hivyo basi kwa nini vikundi vya kiraia vilivyokuwa na mwamko zamani vimefifia baada ya demokrasia kuimarishwa? Kila mtu angetarajia kuona mwamko wa kiraia umeshamiri badala ya kufifia katika mfumo mpya wa kidemokrasia.
Kwa bahati mbaya, sivyo ilivyo. Jumuia nyingi zinakosa viongozi wa kuwashikia mwenge na kuwahamasisha ili watende mambo ambayo yataiwezesha nchi hii iwe mahali bora pa kuishi.
Mwandishi: Anaclet Rweyagura/ DW Dar es Salaam
Mhariri: Daniel Gakuba

Mgombea Urais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Dunia Kajiondoa

Mgombea wa kiti cha Urais wa Fifa Michael van Praag amejiondoa kwenye kinyang'anyiro.
Kujiondoa kwa mwenyekiti huyo wa shirikisho la kandanda la Uholanzi sasa kumewaacha wagombea wawili pekee wanaowania kiti hicho na rais wa FIFA Sepp Blatter.
Van Praag, mwenye umri wa miaka 67, amesema atamuunga mkono Prince Ali Bin Al-Hussein wa Jordan katika uchaguzi huo utakaofanyika tarehe 29 Mei.

Mchezaji wa zamani wa kiungo kutoka Ureno Luis Figo, mwenye umri wa miaka 42,ni mgombea mwingine katika uchaguzi huo.
Blatter,mwenye umri wa miaka 79, anatarajiwa kushinda muhula wake wa tano akiongoza soka duniani. FIFA ina wanachama 209 na kila mmoja ana kura moja.
Vyama vingi vya soka vilionyesha nia ya kumuunga mkono Prince Ali.
Hata hivyo chama cha soka cha Uskochi awali kilikuwa kimesema kitamuunga mkono Van Praag.
Kujiuzulu kwake kumekuja baada ya mgombea mwingine,katibu mkuu wa zamani wa FIFA, mfaransa Jerome Champagne kujiondoa mwezi Februari.
"van Praag anasema kuwa atamuunga mkono Al -Hussein"
Uchaguzi huo utafanyika mjini Zurich katika mkutano mkuu wa kila mwaka wa FIFA.
Mshindi lazima apate theluthi mbili ya kura zote zilizopigwa katika awamu ya kwanza.

Credit to: bbcswahili

Sunday, April 19, 2015

Watu zaidi ya 10 wapoteza maisha Nigeria


Habari toka Nigeria zinazotokana na watu kupoteza maisha, Shirika la Afya Duniani, WHO, linasema inavyoelekea dawa ya kuuwa magugu ndio chanzo cha vifo vya watu 18 vilivyotokea kusini-magharibi mwa Nigeria, bila ya sababu kujulikana.
Katika siku chache zilizopita wakaazi katika jimbo la Ondo wamekufa saa chache baada ya kuhisi macho hayaoni sawasawa na kuumwa na vichwa.
Baadae wanazimia.
Msemaji wa WHO alieleza kuwa ukaguzi uliofanywa hadi sasa kutafuta virusi au bacteria haukugundua kitu.
Alisema kwa sasa mawazo yao ni kuwa vifo hivyo vilisa-babishwa na dawa ya kuuwa magugu.

Monday, January 7, 2013

KITUKO KINGINE CHA MBUNGE MIKE SONKO KUTOKA KENYA.

 
Mike Sonko Mbunge wa Makadara Nchini Kenya mwenye Muonekano tofauti na viongozi wengine alionekana na style tofauti ya nywele kichwani wiki iliyopita.Style hii ya Mini-Mohawk iliandikwa Peace yani Amani. Ni rafiki wa karibu sana wa msanii Jaguar.

Sosi: SamMisago Blog

Monday, December 31, 2012

Happy New Year 2013!!

Tunakushukuruni wafuatiliaji wa blogu hii ya wamtaanitz.com kwa taarifa mbalimbali juu ya jamii yetu ya kitanzania.

Shukrani wote na heri ya Mwaka Mpya 2013!

Wednesday, October 24, 2012

Ndege ya kivita yaua rubani mwanafunzi wa Jeshi la Wananchi TZ



Askari wa JWTZ


Ndege ya kivita ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) imeanguka na kusababisha kifo cha mwanajeshi mmoja na kujeruhiwa mmoja wakati wakiwa katika mafunzo ya kurusha ndege.

Msemaji wa JWTZ, Kanali Kapambala Mgawe, akizungumza na NIPASHE alithibitisha kutokea kwa tukio hilo jana majira ya saa 4:28 asubuhi makao makuu ya kambi ya Jeshi la Anga (Air Wing) eneo la Ukonga, jijini Dar es Salaam.

 

Kanali Mgawe alimtaja mwanajeshi aliyepoteza maisha kuwa ni Kapteni Gatius Magushi ambaye alikuwa na mwenzake wakifanya mazoezi ya kijeshi ya namna ya kurusha ndege.

Alisema marehemu Mgushi wakati wa mafunzo hayo alikuwa na mwenzake kapteni Kwidike ambaye namejeruhiwa na kulazwa katika Hospitali ya Kijeshi ya Lugalo.

Kanali Mgawe alisema wanajeshi hao wakiwa katika mafunzo hayo, baada ya kuwasha ndege, iliruka mita 100 kutoka usawa wa bahari na baada ya muda mfupi ilipata hitilafu na kuanguka.

“Kwa kawaida ndege ikisharuka inapokuwa angani hutakiwa viti vilivyomo katika ndege hiyo kufyatuka tayari kwa marubani hao kuruka kwa kutumia maparashuti,” alisema Kanali Mgawe.

Aliongeza kuwa baada ya viti vya ndege kufyatuka, rubani mmoja hutakiwa huruka kwenda upande wa kushoto na mwingi upande wa kulia.

Alisema kilichotokea ni kwamba viti vya marubani hao vilifunguka pamoja na maparachuti yao yalifunguka, lakini kwa bahati mbaya aliyedondokea upande wa kulia alifikia juu ya paa na alifariki hapo hapo na aliyerukia upande wa kushoto aliangukia  kwenye lami na kujeruhiwa .

Kanali Mgawe alisema hata hivyo, ndege hiyo haijaharibika sana isipokuwa  kifaa kinachotumika kupimia mwendo kasi pamoja na bawa moja vimeharibika.

 
CHANZO: NIPASHE