Tuesday, July 10, 2012

Mashine za kuuza kondomu kufungwa vyuoni.

File:Nkrumah.JPG 
Nkrumah hall UDSM

SHIRIKA linalotoa Elimu na Huduma za Afya, PSI-Tanzania, lina mpango wa kuweka mashine za kuuza kondomu katika maeneo ya vyuo vikuu mbalimbali nchini.
Hatua hiyo inakuja kutokana na kilio cha wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kuomba uwepo utaratibu utakaorahisisha upatikanaji wa kondomu katika Hosteli ya Mabibo.
Akizungumza na Tanzania Daima kwenye Maonesho ya 36 ya Biashara ya Kimataifa yaliyomalizika rasmi jana, Mshauri Mtaalamu wa Programu ya Ukimwi wa shirika hilo, Dk. Alex Ngaiza, alisema kwa sasa wameamua kujikita kusambaza kondomu kwenye maeneo hatarishi ikiwemo vyuo vikuu.
Akifafanua zaidi kuhusu ili alisema wana mpango wa kuhakikisha ATM hizo zinakuwa chini ya serikali za wanafunzi ili mpango huo uweze kuwa endelevu ambapo kwa kuanzia wana mpango wa kupeleka huduma hiyo katika vyuo 20 kikiwamo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
 
Nembo ya IFM

“Kama shirika, tuliguswa na hivi karibuni mmoja wa viongozi wa Serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu cha UDSM (DARUSO) pale alipoiambia kamati ya Bunge kuwa maambukizi ya virusi vya ukimwi chuoni hapo yanachangiwa na tatizo la kutopatikana kondomu kwa urahisi.
Akiitolea mfano Hosteli ya Mabibo, mwanafunzi huyo alisema kuwa kondomu zinapatikana kwenye zahanati ya chuo, hivyo ikishafungwa nyakati za usiku si rahisi kupata kondomu na kushauri kuwe na utaratibu wa kuziweka kwenye maeneo mbalimbali ya hosteli hiyo ikiwa ni pamoja na chooni ili waweze kuzipata kwa urahisi. “Hivyo kutokana na ushauri huo tukaona hatuna budi kuchukua hatua”, alisema Dk. Ngaiza...
Hata hivyo Dk. Ngaiza alikiri kwamba matumizi ya kondomu nchini bado si ya kuridhisha, ingawa kuna mwamko ikilinganishwa na ilivyokuwa huko nyuma.