Shirika la Umeme nchini (Tanesco) limesema zoezi la kuboresha mfumo wa kununua umeme wa LUKU litaendelea kwa mwezi mmoja lengo likiwa ni kuongeza mapato na kubaini wateja wanaolihujumu shirika hilo kwa kuiba umeme.
Akizungumza na NIPASHE jana, Kaimu Meneja Uhusiano wa Tanesco, Adrian Severin, alisema licha wateja wengi kuona zoezi hilo linawaletea usumbufu kwa kupanga foleni kwa muda mrefu, lakini lengo lake ni kuboresha mfumo wa kuuza umeme wa Luku ili kuwahudumia wateja kwa ufanisi na kuwabaini wahujumu.
CHANZO:
NIPASHE