Thursday, August 30, 2012

Ajira Mkapa Foundation...



TAASISI YA BENJAMIN WILLIAM MKAPA HIV/AIDS
kwa kushirikiana na
ABBOTT FUND TANZANIA

TANGAZO LA KAZI LA WATEKNOLOJIA WA MAABARA (FELLOWS)

Katika kuchangia jitihada za Serikali za kuboresha utoaji na upatikanaji wa huduma bora za afya, Taasisi
ya Benjamin William Mkapa HIV/AIDS Foundation (BMAF) imekuwa ikitekeleza miradi mbalimbali
ikiwemo mradi wa ‘Mkapa Fellows’ tokea mwaka 2005.
Katika kuendeleza Mradi huu, Taasisi ya Mkapa Foundation kwa kushirikiana na Abbott Fund Tanzania
inatekeleza mradi wa kuimarisha huduma za afya kwenye Maabara za Hospitali za Mikoa. Moja ya
malengo ya mradi huu ni kuongeza wataalam wa maabara (Fellows) katika maabara za Mikoa 10
ambazo zimeboreshwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na Abbott Fund
Tanzania, na kuwa za kisasa na zenye vitendea kazi vya kutosha.
Katika kutekeleza mradi huu, Wateknolojia wa Maabara 26 wamekwishaajiriwa na kupangiwa kazi katika
hospitali za Mikoa ya Lindi, Mtwara, Pwani (Hosptali ya Tumbi), Tabora na Kigoma. Awamu ya pili ya
mradi inalenga kuajiri Wateknolojia wa Maabara 34 ambao watapangiwa kufanya kazi katika
Hospitali za Mikoa nane (8) kama inavyoainishwa kwenye jedwali hapa chini:

HOSPITALI YA MKOA IDADI YA WATEKNOLOJIA WANAOHITAJIKA
MARA 6
KAGERA 6
SINGIDA 6
RUKWA 6
SHINYANGA 6
TABORA 2
KIGOMA 1
PWANI 1
JUMLA 34

Izingatiwe kwamba:
• Ajira ndani ya mradi huu itatolewa kwa mkataba wa miezi kumi na mbili,(12) na mara baada ya
kukamilika kipindi hiki, waajiriwa wote katika mradi huu watatakiwa kujiunga katika utumishi wa
umma kulingana na taratibu na kanuni za Serikali za Ajira
• Watumishi waliopo kwa sasa katika ajira ya utumishi wa umma, au katika Taasisi/Vyuo vya
mashirika ya dini (FBOs) hawaruhusiwi kuomba nafasi hizi.
• Wataalamu wenye umri chini ya miaka 45 wanashauriwa kuomba nafasi hizi za kazi, na
watakuwa na fursa ya kupata ajira serikalini kwa masharti ya kudumu na pensheni.
Waajiriwa wote (Mkapa Fellow) katika Mradi huu watapata mafao yafuatayo:
• Mishahara kulingana na ngazi zilizoainishwa katika Muundo wa Utumishi wa Umma katika Sekta
ya Afya
• Posho ya nyumba, mafunzo kazi pamoja na ‘‘laptop’’ /kompyuta
• Mafao ya matibabu
• Kiinua mgongo baada ya kumaliza miezi 12 ya mkataba
• Baada ya kukamilisha kipindi cha mkataba watakuwa sehemu ya ‘‘Mkapa Fellows Alumni’’


Maombi yote yaambatanishwe na:
1. Barua ya maombi ya kazi, ikipendekeza hospitali mwombaji anayopendelea kupangwa kazi, na
pia aonyeshe ridhaa ya kujiunga na utumishi wa umma, baada ya mkataba wa miezi 12
kumalizika.
2. Nakala ya cheti cha Taaluma na cheti cha kidato cha 4 na 6 (iwapo anacho), na viwe
vimethibitishwa na Hakimu au Wakili.
3. Picha mbili (2) – saizi ya Pasipoti na maelezo binafsi (CV), ikionyesha umri, anuani kamili na
namba ya simu ya kiganjani, pamoja na anuani/ namba ya kiganjani ya wadhamini wako.
Mwisho wa kupokea maombi haya ni tarehe 30 Augosti 2012

Maombi yote yatumwe kwa:
Afisa Mtendaji Mkuu, Benjamin William Mkapa HIV/AIDS Foundation, SLP 76274, Kiwanja Na. 372,
Barabara ya Chole, Masaki - Dar es salaam
Au kwa Barua pepe : info@mkapahivfoundation.org
Tangazo hili linapatikana pia katika tovuti ya:
www.mkapahivfoundation.org