Tuesday, July 24, 2012

Dk. Ulimboka kurudi nchini hivi karibuni


Dr Ulimboka mwenye mic.

Afya ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Stephen Ulimboka, aliyepelekwa Afrika Kusini kwa matibabu imeendelea kuimarika na kwa mujibu wa familia yake anatarajiwa kurejea nchini mwishoni mwa mwezi huu.




Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mmoja wa familia yake aliliambia NIPASHE jana kuwa, Dk. Ulimboka anatarajia kurudi nchini muda wowote kuanzia sasa kutokana na hali yake kuendelea kuwa nzuri.



Wiki iliyopita Dk.Ulimboka alianza kufanya mazoezi mepesi mepesi huko Afrika Kusini anakotibiwa.



Dk.Ulimboka, aliyetekwa Juni 26, mwaka huu, alipigwa na kuumizwa mwili mzima, aling’olewa meno pamoja na kucha na watu wasiojulikana na baadaye mwili wake kuokotwa na msamaRlia mwema maeneo ya Mabwepande nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.



Baada ya kitendo hicho, Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), kiliamua kumpeleka Dk. Ulimboka Afrika Kusini kwa matibabu.