Kipre Tchetche
MSHAMBULIAJI wa Azam FC, Kipre Tchetche, anajipanga kufunga mabao mengi katika michuano ya Kombe la Kagame ili kuipa mafanikio timu yake na kuthibitisha ubora wao kwenye ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
Tchetche ambaye ni raia wa Ivory Coast, Watanzania wanamkumbuka kwa mabao yake ya dakika za mwishoni alipokuwa akiingia kipindi cha pili wakati akichezea timu ya taifa lake katika michuano ya Kombe la Chalenji mwaka juzi.
Akizungumza na Mwanaspoti, Tchetche, ambaye alifunga mabao sita kwenye Ligi Kuu Bara msimu uliopita, alisema: "Kazi yangu ni kufunga, nataka kufunga mabao mengi kadiri niwezavyo. Kwa sasa naisubiri Kagame ili kuipa mafanikio timu yangu.
"Naamini naweza kufanya hivyo kwa ushirikiano wa wenzangu."
Katika michuano ya Kombe la Ujirani Mwema inayoendelea hapa Zanzibar, amefunga bao moja.
Tchetche, ambaye yumo kikosini hapo na pacha wake, Kipre Bolou, ndiye mchezaji anayetarajiwa kuing'arisha safu ya ushambuliaji ya Azam pamoja na George Odhiambo Blackberry, John Boko Adebayor, Mrisho Ngassa na Gaudence Mwaikimba.