Picha hii ni cover ya wimbo wa Happy Day. Picha kwa hisani ya ActionRec Blog. |
Msanii anayekuja kwa kasi katika muziki huu wa kizazi kipya wa kufokafoka anayejulikana kwa jina la Mequiz as Brain aliachia wimbo huu siku chache zilizopita. Msanii huyu aliongea na Blog hii nakusema kuwa atafanya mambo mengi mwaka huu wa 2016 katika tasnia hii ya muziki pia alisema kuwa ataachia video ya wimbo huu siku zijazo.
Wimbo huu kawashirikisha wakali wa muziki wa kizazi kipya Mjini hapa Kahama toka kundi la Nyasubi Texas na kufanya kazi na studio za Action Records. Kuupakua wimbo huu bonyeza link hii >>>HaPa<<<