Friday, August 24, 2012

Zoezi la Uandikishaji wa Watu wa Makundi maalumu (Walemavu) litafuata...:NIDA




Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), imesema inasubiri kumalizika kwa zoezi la sensa ya watu na makazi ndipo uhandikishaji wa watu wa makundi maalumu (Walemavu) litafuata.

Akitoa taarifa hiyo jana, Ofisa Habari wa Nida, Rosi Mdami, alisema kwa sasa kinachosubiriwa ni kumalizika kwa zoezi la sensa ya watu na makazi ndipo wataanza kuandikishwa watu wenye wa makundi maalumu.

Alisema kwa sasa hawawezi kuendesha mazoezi mawili kwa wakati mmoja hivyo wanasubiri kumalizika kwa zoezi la sensa.

“Ndugu mwandishi, kwa sasa unafahamu kuna zoezi la Sensa linaendelea, si vyema tukaanza zoezi la uwandikishaji wa vitambulisho huku zoezi hili halijamalizika, tunasubiri sensa imalizike kwanza,” alisema Mdami.

Aidha Mdami alisema Nida inatambua umuhimu wa zoezi la kuwaandikisha watu wa makundi maalumu hivyo hawawezi kuwasahau kwa kuwa na wao wanahaki ya kupata vitambulisho hivyo.