Sunday, June 17, 2012

Mashamba Darasa 303 yaanzishwa Singida..

 MKOA wa Singida  umeanzisha mashamba  darasa 303 katika maeneo mbalimbaliya vijijini kama  njia mojawapo ya kukabiliana na  tatizo la  upungufu wawataalamu wa ugani.

Mshauri wa kilimo katika Sekretarieti ya mkoa huo, Deusdedit Rugangiraamesema  hivi  sasa kunawataalamu  wa ugani 80 tu kati ya 420 wanaohitajika ili  kuwezakuwahudumiavyema wakulima  vijijini.

Alisema  kutokana na  hali hiyo, wameona  kuna haja ya kuanzisha mashamba darasa hayo, ili yawawezeshe wakulima wa maeneo  husika kutembelea na kujifunza juu ya  kilimo bora.

Rugangira alisema, lengo ni kuhakikisha kuwa wakulima wanajengautamaduni wa  kuzingatia ushauri wa kitaalamu kwa kutumia mbegu bora,mbolea na  kulima kwa wakati muafaka  ili kuongeza tija.

Source: Mwananchi