Sunday, April 19, 2015

Watu zaidi ya 10 wapoteza maisha Nigeria


Habari toka Nigeria zinazotokana na watu kupoteza maisha, Shirika la Afya Duniani, WHO, linasema inavyoelekea dawa ya kuuwa magugu ndio chanzo cha vifo vya watu 18 vilivyotokea kusini-magharibi mwa Nigeria, bila ya sababu kujulikana.
Katika siku chache zilizopita wakaazi katika jimbo la Ondo wamekufa saa chache baada ya kuhisi macho hayaoni sawasawa na kuumwa na vichwa.
Baadae wanazimia.
Msemaji wa WHO alieleza kuwa ukaguzi uliofanywa hadi sasa kutafuta virusi au bacteria haukugundua kitu.
Alisema kwa sasa mawazo yao ni kuwa vifo hivyo vilisa-babishwa na dawa ya kuuwa magugu.