Sunday, July 15, 2012

Ujumbe wa Leo Kagame Cup toka simba..

 http://kandanda.galacha.com/wp-content/themes/LondonLive/thumb.php?src=http://kandanda.galacha.com/wp-content/uploads/2012/06/cirko.jpg&w=340&h=192&zc=1&q=100
Milovan Cirkovic

Kocha Mkuu wa Simba, Milovan Cirkovic amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kujionea wenyewe uwezo wa timu yao.
Alisema ana imani kubwa na kikosi chake kutokana na maandalizi waliyopata kwenye mechi za kujipa nguvu zikiwamo za michuano ya Urafiki iliyofikia tamati Alhamisi wakitwaa ubingwa kwa kuifunga Azam FC.
“Nawasihi wapenzi na mashabiki wa Simba, wajitokeze kwa wingi kuishangilia timu yao kama walivyofanya katika Ligi Kuu iliyopita hadi kutwaa ubingwa, ” alisema Milovan.
Mechi hiyo kati ya Simba na URA, itatanguliwa na mechi nyingine ya kundi hilo kati ya Vita Club ya DR Congo dhidi ya Ports ya Djibouti, itakayoanza saa 8 mchana kwenye uwanja wa Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.