Sunday, July 1, 2012

Mengi, Malasusa wamtembelea Dk. Ulimboka


mengi
Bw. Mengi
Juzi mchana na jana asubuhi kwa nyakati tofauti Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT) Regnald Mengi na Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Alex Malasusa walifika hospitalini hapo kumjulia hali Dk. Ulimboka.
Mengi alifika hospitalini hapo juzi saa saba mchana ambapo alizungumza na viongozi wa Chama cha Madaktari (MAT) akiwemo Mwenyekiti wao Dk. Namala Mkopi kabla ya kumwona Dk. Ulimboka.
http://profile.ak.fbcdn.net/hprofile-ak-snc4/50556_118118024865483_4207516_n.jpg
Askofu Malasusa

Baada ya kumwona mgonjwa, Mengi hakutaka kuzungumza na waandishi wa habari waliokuwepo kwenye viunga vya hospitali hiyo kisha kuondoka.
Kama ilivyokuwa kwa mwenyekiti wa MOAT, askofu Malasusa naye hakuzungumza na waandishi wa habari baada ya kumwona mgonjwa huyo jambo lililoacha maswali mengi kuhusu hali ya Dk. Ulimboka.
Dk. Ulimboka alitekwa na kupigwa usiku wa Juni 28 na watu aliodai ni usalama wa taifa na kupelekwa katika msitu wa Mabwepande na tangu siku hiyo hali yake imeendelea kusuasua.
Awali mmoja wa madaktari wanaolinda mlango wa chumba cha wagonjwa mahututi alimolazwa Dk. Ulimboka alisema idadi kubwa ya wanasiasa kwa nyakati tofauti walifika kumjulia hali lakini walizuiwa.
Bila kuwataja wanasiasa hao, daktari huyo alisema wapo wanasiasa wanaowapigia simu viongozi wa MAT na jumuiya kutaka kufanya hivyo bila mafanikio huku akisisitiza kwamba kadri hali inavyozidi kuwa mbaya ni madaktari pekee watakaoruhusiwa kuingia kwenye chumba hicho.

Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima